Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 11:19

Kongo yaadhimisha miaka 54 ya uhuru wake.


Patrice Lumumba, waziri mkuu wa Congo akitia saini tangazo la uhuru mjini Leopodville, Congo. Kulia kwake ni waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji Gaston Eyskens, aliyetia saini kwa niaba ya Ubelgiji. Ubelgiji iliitawala Congo kwa miaka 70.
Patrice Lumumba, waziri mkuu wa Congo akitia saini tangazo la uhuru mjini Leopodville, Congo. Kulia kwake ni waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji Gaston Eyskens, aliyetia saini kwa niaba ya Ubelgiji. Ubelgiji iliitawala Congo kwa miaka 70.

Maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Kongo yamesherehekewa kwa kuwaenzi wanajeshi wa nchi hiyo kutokana na ushindi wao dhidi ya makundi ya wapiganaji.Hata hivyo rais Joseph kabila ametowa mwito kwa ajili ya mshikamano wa wananchi wote kutokana na vitisho vya kiusalama.

Baada ya miaka minne ya kutoandaa sherehe zozote kutokana na madhimisho ya kikukuu ya uhuru wa Kongo.Mwaka huu rais Kabila amesema maadhimisho ya uhuru wa Kongo ni kwa ajili ya kuwaenzi wanajeshi wa FARDC.Kwenye hotuba wa dakika 15 kwa taifa,rais Kabila amesema kwamba hatua hiyo inatokana na ushindi wao dhidi ya makundi ya wapiganaji huko Kivu.

Alisema "wanajeshi wetu wanastahili heshima hizi kutokana na ushindi wa aina yake dhidi ya makundi yote ya waasi yakiwemo yale kutoka nje,yale ya kitaifa na watu wa nia mbaya ambao wanataka mgawanyiko na wa raia wetu".

Rais Kabila amesema bado watu wanaopanga njama ya kuigawa Kongo wako imara kwa hiyo nilazima kuweko na mshikamano wa wakongomani wote.

"Ijapokuwa kuridhishwa na mafanikio ya hivi sasa ambayo ni halali,lakini tuwe katika angalisho kubwa, kwa sababu adui bado yuko anatuzunguka na hajaacha njama yake ".

Hotuba hiyo ya rais Kabila imekuja wakati ambapo raia wanasubiri kwa hamu serikali ya mseto alioahidi miezi minane iliyopita,kufuatia kongamano la kitaifa.Rais Kabila amesema bila shaka atatekeleza mazimio yote ya kongamano hilo la kitaifa lakini bila haraka yeyote.

"Nimehakikisha upya nia yangu ya kutekeleza maazimio yote ya kongamano hilo,lakini kwa mipangilio na bila haraka yeyote.Nimehimiza pia kila mmoja wetu wanasiasa,wafanya biashara na mashirika ya kiraia ili kufanya kazi kwa ajili ya kuwaweka pamoja raia wetu ".

Bila kuzitaja majina rais Kabila alipongeza pia juhudi za nchi rafiki za DRC katika kurejesha amani ya kudumu nchini mwake.Na aliahidi kujenga mnara wa kumbukumbu kwa ajili ya wanajeshi wote waliopoteza maisha yao kwa ajili ya ulinzi wa mipaka ya Kongo.

Wanajeshi wa Congo katika gwaride ya sherehe za uhuru June 2014
Wanajeshi wa Congo katika gwaride ya sherehe za uhuru June 2014

Kwenye hotuba yake hiyo rais Kabila aligusia pia kufukuzwa kwa raia wa Kongo wanaoishi Brazzaville katika kile alichokiita kuwa ni hali isiyo ya kibinadamu.Rais kabila amewatolea mwito raia wote wa Kongo wanaoishi nje ya nchi warejee kwa hiari yao wenyewe kuchangia katika ujenzi wa taifa lao.

Gwaride kubwa la kijeshi lilifanyika mjini Kinshasa ambako mwenyewe rais Kabila na mkewe walihudhuria.Maadhimisho ya miaka 54 ya uhuru wa Kongo yalifanyika pia katika miji yote mikubwa ya Kongo.

XS
SM
MD
LG