Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 11:38

Wanadiplomasia wa magharibi watoa wito kwa Iraq kuungana.


Polisi wa Iraqi wakifanya doria kaskazini mwa Baghdad, Iraq, Juni 26, 2014.
Polisi wa Iraqi wakifanya doria kaskazini mwa Baghdad, Iraq, Juni 26, 2014.

Wanadiplomasia wa juu kutoka nchi za magharibi wanatilia mkazo mzozo wa Iraq na kuzidi kutoa wito kwa nchi hiyo kuungana katika wakati ambapo wanamgambo wa Sunni wanaendeleza mashambulizi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alifanya ziara ya Baghdad Alhamisi ambako alikutana na waziri mkuu wa Iraq Nouri Al-Maliki na kupanga kufanya mazungumzo na Massoud Barzani rais wa eneo linalojitawala la Wakurdi.

Hague alisema Iraq “wanakumbana na hatari inayotishia kugawika kwa nchi hiyo” na kwamba umoja wa kisiasa ndio jambo pekee la muhumu ili kuweza kupambana na changamoto hiyo.

Huko Paris waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry. Fabius alisema Iraq inapambana na hali ngumu lakini wanategemea Iraq kuungana.

XS
SM
MD
LG