Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:40

Mlipuko mwingine wa bomu waua watu 21 Nigeria.


Mlipuko wauwa watu 21 mji mkuu wa Nigeria wa Abuja
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:51 0:00

Polisi wa Nigeria wanaeleza kwamba takriban watu 21 wameuwawa na 52 kujeruhiwa siku ya Jumatano wakati bomu lililipuka katika mtaa wa maduka ya biashara ulojaa watu katika mtaa wa matajiri mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria.

Mlipuko ulitokea kiasi ya saa kumi jioni saa za Nigeria wakati kulikuwepo na idadi kubwa ya watu madukani.

Blessew Marta alikua anauza njugu nje ya soko. Anasema alirudi nyumbani dakika tano tu kabla ya bomu kulipuka, lakini dada zake wawili na rafiki yake walokua wanauza ndizi hawakunusurika.

"Kabla ya hata kuweza kurudi nakuta hakuna aliyenusurika, hivi sasa mahala hapa imeteketea na kugeuka jivu. Hakuna kati ya wauzaji ndizi walonusurika, wamefariki hivi hivi."

Polisi inaeleza kwamba imewakamata watu ambao huwenda walihusika na mlipuko, lakini kwa wakati huu kaijawalaumu kundi la Boko Haram ambalo linalaumiwa kufanaya mashambulizi kama hayo na kwisha wauwa zaidi ya watu elfu mbili mwaka huu pekee.

Msemaji wa polisi Franck Mbah anasema

"Niwazi ni tukio la mlipuko, maelezo zaidi juu ya aina ya chombo kiliochotumiwa au kutengenezwa kufanya mlipuko huo haijulikani bado."

Uwasi uanoendelea kwa miaka mitano sasa huko Nigeria, aghlabu hufanyika kaskazini mashariki katika majimbo matatu amabyo yako chini ya utawala wa dharura kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Lakini inavyoonekana uwasi unapanuka na mbinu zake zinabadilika kila mara ikiwa ni pamoja na utekaji nyara wa wanawake na wasichana wengi.

Baada ya miaka miwili ya utulivu katika mji mkuu wa Abuja , kumeshatokea milipuko mitatu ya bomu tangu mwezi wa April na kusababisha zaidi ya vifo vya watu 100. Kundi la Boko Haram limedai kuhusika na shambulio la kwanza la bomu mjini Abuja mwaka huu na kutishia kutakuwepo na milipuko zaidi.

XS
SM
MD
LG