Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 20:01

Waandishi Al Jazeera wahukumiwa miaka saba jela.


A screenshot of Aljazeera channel showing anti-government protests in the Egyptian port city of Alexandria on Aug. 30, 2013
A screenshot of Aljazeera channel showing anti-government protests in the Egyptian port city of Alexandria on Aug. 30, 2013
Mahakama moja ya Misri imewahukumu waandishi watatu wa Al Jazeera kifungo cha miaka saba jela kwa mashitaka ya kuwaunga mkono Muslim Brotherhood chama kilichopigwa marufuku na kusambaza habari za uongo, kesi ambayo imelaaniwa kimataifa.

Waandishi hao watatu walihukumiwa leo mjini Cairo ni pamoja na raia wa Australia Peter Greste , raia wa Canada mwenye asili ya Misri Mohamed Fahmy na raia wa Misri Baher Mohamed ambaye alihukumiwa miaka mitatu zaidi kwa makosa mengine.

Al Jazeera siku zote wamekana makosa hayo dhidi ya wafanyakazi wao, kaimu Mkurugenzi Mostefa Souag alisema hukumu hiyo inashangaza na kusema Aljazeera itaendelea na kampeni yake ya kimataifa ili waandishi wake waachiwe huru.

Mkurugenzi mtendaji wa idhaa ya kiingereza ya Aljazeera Al Anstey alisema hukumu hizo zilitolewa licha ya kutokuwepo na ushahidi kuunga mkono mashitaka hayo na kusema matokeo ya maana ya kesi hiyo itakuwa ni kutengua maamuzi hayo.
XS
SM
MD
LG