Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:26

Kerry azungumzia demokrasia, Irak na wamisri


Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry, (kushoto), akizungumza na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi kabla ya mkutano wao katika ikulu ya rais Cairo, Misri, June 22, 2014.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry, (kushoto), akizungumza na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi kabla ya mkutano wao katika ikulu ya rais Cairo, Misri, June 22, 2014.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry amekutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi wakati wa ziara yake ya ghafla isyotangazwa huko Mashariki ya Kati na kuzungumzia juu ya masuala ya demokrasia na hali ya vita Irak.

Kerry aliwasili jana Cairo kwa mkutano wa kwanza na viongozi wa juu pamoja na kiongozi mpya wa Misri, tangu nchi hiyo ifanye uchaguzi wa rais mwezi Mei.

Wakati wa ziara hiyo, mwanadiplomasia huyo wa Marekani alieleza juu ya uhusiano wa muda mrefu uliokuwepo kati ya Washington na Cairo, alisisitiza kwamba mataifa hayo mawili yatafanya kazi pamoja katika kupambana na vitisho vya ugaidi.

Kerry pia alitoa wito kwa viongozi wa Misri kuheshimu haki za kimataifa za uhuru wa kujieleza na uhuru wa kukusanyika. Mwito wake wa uhuru kwa vyombo vya habari unatolewa wakati mahakama moja huko Misri inatazamiwa kutoa uwamuzi Jumatatu katika kesi inayowahusisha waandishi wa habari watatu wa kituo cha televisheni cha Al-Jazeera wanaoshutumiwa kwa kuripoti habari za uongo na kulisaidia kundi lililopigwa marufuku nchini humo la Muslim Brotherhood

Akizungumza mjini Cairo siku ya Jumapili Kerry alionya kuhusu hatari za wapiganaji wa kisunni kuendelea kunyakua maenero zaidi ya Iraq, lakini pia alitoa wito kwa viongozi wa Baghdad kuacha kando tofauti Zao za kidini na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi wake
XS
SM
MD
LG