Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:53

Wanamgambo wa kiislam wazidi kusonga mbele Iraq.


Wapiganaji wa Islamic State of Iraq na Levant (ISIL) wakilinda kizuizi cha bara bara huko Mosul, kaskazini mwa, Juni 11, 2014.
Wanamgambo wa kiislam wanaendelea kuchukua maeneo zaidi huko Iraq wakati Marekani inatafakari namna ya kujibu hatua hizo za waasi.

Maafisa wanasema wanamgambo waliteka miji ya Jalawla na Saadiyah katika eneo la kikabila lililogawanyika la mashariki la Diyala Alhamisi usiku.

Kundi la wanamgambo wa ISIL au Islamic State of Iraq limeteka eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq na linaendelea kwenda kuelekea kwenye mji mkuu.

Rais Barack Obama alisema Ijumaa kwamba anaangalia kila uwezekano na kuamua jinsi gani ya kujibu juu ya mzozo huu unaoendelea kuzorota wa Iraq.

“Tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba watu hawa wenye msimamo mkali hawapati nafasi ya kudumu huko Iraq au Syria” alisema Obama.

Maafisa wa Marekani wameongea kwa masharti ya kutotajwa majina wakisema mambo yanayofikiriwa ni pamoja na uwezekano wa mashambulizi ya ndege za Marekani zisizotumia rubani Drone.
XS
SM
MD
LG