Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:26

Wapenzi wa kandanda duniani waelekeza macho yao Brazil.


Wacheza carnival wakicheza samba huko Sao Paulo, Brazil.
Wacheza carnival wakicheza samba huko Sao Paulo, Brazil.
Wapenzi wa kandanda duniani wanaelekeza macho yao brazil leo ambako fainali za kombe la duniani zinaanza kwa mechi kati ya wenyeji Brazil na Croatia – lakini wabashiri wanatarajia kuwa Brazil itaibuka mshindi.

Serikali imetumia dola billioni 11.5 kutayarisha mashindano haya yatakayo fanyika kwa mwezi mmoja kwa kujenga na kuviboresha viwanja katika miji kumi na miwili ikishirikisha timu 32 .

Waandamanaji wameandamana leo, wakiendelea kuikosoa serikali kwa jinsi ilivyotumia pesa vibaya badala ya kushughulikia mambo mengine muhimu. Mashindano haya yataanza kwa sherehe za ufunguzi huko Sao Paulo kabla ya Brazil kupambana na Croatia.

Timu hii wenyeji inajaribu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita na mara ya kwanza tangu 2002. Timu zingine zinazopewa nafasi ya kushinda kombe hilo ni pamoja na Argentina, Spain, na Ujerumani ambayo kwanza lazima ishinde katika kundi liitwalo “kundi la kifo.’
XS
SM
MD
LG