Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 07:00

Mapigano yazuka baina ya wanajeshi wa DRC na Rwanda.


Wanajeshi wa Congo wakitoa ulinzi huko Walikale.
Maafisa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanasema wanajeshi wake wamepambana na wanajeshi wa nchi jirani ya Rwanda. Maafisa hao wanasema wanajeshi wa Congo walianza mapigano hayo mapema Jumatano baada ya majeshi ya Rwanda kuvuka mpaka na kumteka nyara mwanajeshi wa Congo.

Mapigano hayo ya alfajiri katika eneo la Kibumba lililoko mkoa wa North Kivu mashariki mwa nchi yalidumu kwa saa nne. Hakuna maelezo yoyote juu ya majeruhi.

Katika mtandao wake wa twitter, tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO imesema inapeleleza tukio hilo. Majehsi hayo ya MONUSCO yakisaidiana na jeshi la Congo yalifanikiwa kulidhibiti kundi la waasi wa M23 katika mkoa huo wa North Kivu mwaka jana . Rwanda imekanusha madai ya Umoja wa Mataifa kuwa iliwaunga mkono waasi hao.
XS
SM
MD
LG