Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 22, 2025 Local time: 13:22

Imam Mohamed Iddriss auwawa Kenya.


Mhubiri wa kiislam mwenye ushawishi mkubwa, Mohamed Idris 64, na mwenyekiti wa barzala la mMaimama Kenya, ameuwawa huko Mombasa, Kenya Juni 10, 2014.
Mhubiri wa kiislam mwenye ushawishi mkubwa, Mohamed Idris 64, na mwenyekiti wa barzala la mMaimama Kenya, ameuwawa huko Mombasa, Kenya Juni 10, 2014.
Watu wenye silaha wamemuuwa kiongozi wa kiislam Mombasa akiwa ni kiongozi wanne wa kidini kuuwawa mjini humo katika miaka miwili iliyopita.

Polisi wanasema sheikh Mohamed Iddriss mwenyekiti wa baraza la Maiman na Wahubiri Kenya alipigwa risasi na kuuwawa nje ya msikiti jumanne asubuhi.

Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji hayo. Wachunguzi wanasema sheikh huyo mwenye msimamo wa kadri ametishiwa mara kadhaa na vijana wa kiislam wenye msimamo mkali na alikuwa na wasi wasi juu ya maisha yake.

Viongozi watatu wa kiislam waliouwawa mapema katika mji huo walishutumiwa kwa kuwa na mahusiano na kundi la alshabab lenye mahusiano na alqaeda lililopo Somalia.

Vikosi vya kijeshi vya Kenya viko Somalia vikipambana na wanamgambo wa Somalia ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi Kenya hasa lililokuwa kubwa sana la maduka ya kifahari ya westgate huko Nairobi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 60 waliuwawa.
XS
SM
MD
LG