Mahakama kuu inapanga Ijumaa kutoa maamuzi kama iwapo matokeo ya uchaguzi yatangazwe hadharani au kura zihesabiwe tena. Matokeo ya awali yamemuweka Bi. Banda nyuma ya mpinzani wake Peter Mutharika.
Bi.Banda anasema uchaguzi ulijaa ubadhirifu, ikiwemo pamoja na wizi wa kura na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.
Ameliambia shirika la habari la reuters kwamba atakubali maamuzi ya mahakama kuu, akifahamu fika kuwa amejaribu kutetea haki za wamalawi kwa kuhakikisha kuwa kiongozi anachaguliwa kwa haki na utaratibu wa heshima.
Bi.Banda ameamuru uchaguzi mpya uitishwe katika kipindi cha siku 90 na kusema hatakuwa mgombea. Lakini mahakama kuu imebatilisha maamuzi yake pale chama kikuu cha upinzani kilipowasilisha malalamiko.