Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:07

Hillary Clinton atoa kitabu akieleza kujivunia kazi yake.


Hillary Clinton akizungumza mjini Washington.
Hillary Clinton akizungumza mjini Washington.
Hillary Clinton ameandika katika kitabu chake akieleza kuwa ana sikia fahari kubwa kwa yale aliyofanya akiwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Kitabu cha Clinton “Hard Choices” kinatoka Juni 10 wakati uvumi ukiendelea kuongezeka juu ya uwezekano wa yeye kugombea urais 2016.

Katika waraka wa mwandishi uliotolewa jumanne Clinton anasema anatamani angerudi nyuma na kuangalia upya baadhi ya maamuzi yake wakati akifanya kazi kama mwanadiplomasia wa juu wa Marekani.

Lakini anasema serikali ilihataji kufanya vizuri zaidi baada ya mashambulizi ya kigadi ya 2001, vita vya Afghanistan na Iraq na kudorora kwa uchumi na anaamini ilifanya .

Wakosoaji wameelezea kwamba miaka minne ya Clinton kwenye wizara ya mambo ya nje kuwa ilikosa mafanikio makubwa. Warepublikan pia wameuliza juu ya jinsi alivyosimamia mashambulizi ya Septemba 11, 2012 ambayo yaliuwa wamarekani wanne katika mji wa Benghazi nchini Libya.
XS
SM
MD
LG