Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 22:05

Marekani yapeleka msaada wa wataalam wa kijeshi Chad.


Raia wa Nigeria wakiandamana wakidai kuachiwa kwa wasichana waliotekwa na Boko Haram huko Abuja Nigeria.
Rais wa Marekani Barack Obama amepeleka wafanyakazi 80 wa jeshi la Marekani nchini Chad ili kusaidia kutafuta zaidi ya wasichana wa shule 250 waliotekwa na wanamgambo wa kiislam mwezi uliopita katika nchi jirani ya Nigeria.

Katika barua jumatano kwa bunge la Marekani, Bw.Obama amesema wafanyakazi hao wa Marekani watasaidia operesheni za kijasusi, upelelezi na ndege za kijeshi za upelelezi katika anga ya kaskazini mwa Nigeria na maeneo yanayozunguka. Alisema jeshi hilo litaendelea kubaki Chad kutafuta watoto hao mpaka itakapokuwa haihitajiki tena.

Wasichana hao walitekwa na Boko Haram Aprili 14 kutoka kwenye shule ya bweni katika eneo la ndani sana karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon, Niger na Chad. Mahali walipo bado hakujulikani.
XS
SM
MD
LG