Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:34

Marekani yaahidi dola millioni 300 kwa Sudan Kusini.


Mkuu wa masuala ya kibinadam Valerie Amos na waziri wa mambo ya nje wa Norway Borge Brende katika mkutanio wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Sudan Kusini huko Oslo Norway.
Marekani inaahidi kiasi kingine cha dola milioni 300 katika misaada ya kibinadamu kwa Sudan kusini , ambapo umoja wa mataifa unasema watu milioni 4 wako katika hatari ya kukumbwa na njaa.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema Marekani inajibu haraka mahitaji ya chakula ikiwa ni pamoja na mahitaji ya chakula kwa watoto walio na utapia mlo.

Marekani ni mfadhili mmoja wa juu kwa Sudan Kusini na kutoa zaidi ya dola milioni 434 tangu mwaka jana.

Lakini wizara ya mambo ya nje inasema msaada huo unaweza kuwa na maana kama serikali na upinzani ukiacha kupigana na kuweka vikwazo kwa usambazaji.
XS
SM
MD
LG