Mlipua mabomu wakujitoa muhanga ameuwa watu wasiopungua wanne jumapili katika eneo la wakristo katika mji wa kaskazini mwa Nigeria wa Kano.
Polisi wanasema mlipuko huo ulitokea katika mtaa ulio na baa nyingi na migahawa.
Hakuna aliyedai kuhusika lakini shuku inaelekea kwa kundi la Boko Haram kundi la wanamgambo wa kiislam wanaotumia ugaidi kujaribu kuunda taifa la kiislam lenye msimamo mkali huko kaskazini mwa Nigeria.
Boko Haram inashikilia wasichana wa shule 276 ambao waliwateka kijijini mwezi uliopita.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan na viongozi wengine barani Afrika wamehudhuria mkutano ulioandaliwa na Ufaransa mjini Paris Jumamosi juu ya njia za kupambana na magaidi.