Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:52

Obama afungua jumba la makumbuso la mashambulizi ya Septemba 11


Picha ya jengo jipya la makumbusho ya Septemba 11 huko New york.
Picha ya jengo jipya la makumbusho ya Septemba 11 huko New york.
Makumbusho mapya yanayoeleza yale yaliyotokea wakati wa mashambulizi ya Septemba 11 litafunguliwa kwa watu wote wiki ijayo baada ya kufunguliwa na Rais Barack Obama siku ya Alhamisi May 15 2014.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema makumbusho hayo yanatarajiwa kufunguliwa kwa umma wiki ijayo.

Makumbusho hayo yaliyogharimu dola milioni 700 na mnara wa kumbu kumbu yamejengwa kwa miaka kadhaa . Ukamilishaji wake siku zote umekumbwa na mizozo juu ya ujenzi wake, kuchelewesha kazi na mpaka leo kama ikiwa mabaki ya miili ya wale wasiotambuliwa yazikwe chini ya jengo hilo au juu.

Makumbusho hayo yako karibu na chini ya ardhi yakienda mpaka kwenye eneo la vyuma ambalo kuliwekwa jengo la World Trade Centre. Vyuma vikubwa vilivyotoka kwenye jengo lililoharibiwa vinaonyeshwa pamoja na vitu mbali mbali vya makumbusho ya mashambulizi hayo.
XS
SM
MD
LG