Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:39

Wanaotaka kujitenga Ukraine wadai asilimia 89 wapiga kura kudai kujitawala Donetsk.


Wajumbe wa tume ya uchaguzi wakihesabu kura huko Donetsk, Ukraine, May 11, 2014.
Wajumbe wa tume ya uchaguzi wakihesabu kura huko Donetsk, Ukraine, May 11, 2014.
Waandaji wa maandamano ya Jumapili ya kura ya maoni kuhusu uhuru katika mkoa wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk wanasema asilimia 89 ya wale wanaopiga kura walipiga kura kutaka kujitenga na ukraine.

Matokeo hayo yalikuja kwa mshangao si tu kwasababu ya idadi ya juu lakini ni kwasababu yalitangazwa saa tatu tu baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa na baada ya waandishi kuambiwa kwamba hayatakuwa tayari .

Waliojitenga wanasema asilimia 10 walikataa uhuru na kwamba waliojitokeza walikuwa ni asilimia 75. Matokeo ya awali haiwezekani yakathibitishwa kwasababu hakukuwa na wakaguzi wa kimataifa huko Donetsk.
XS
SM
MD
LG