Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:11

Waziri Kerry ziarani Afrika.


John Kerry akifanya mahojiano na Vincent Makori wa VOA.
John Kerry akifanya mahojiano na Vincent Makori wa VOA.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ameanza ziara yake barani Afrika kwa mazungumzo yaliyolenga kuzuia ghasia Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Kituo cha kwanza cha ziara yake kitakuwa Addis Ababa ambapo atakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Ethiopia , Uganda na Kenya kuzungumzia mzozo wa Sudan Kusini.

Jumanne afisa wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema Kerry atatoa ujumbe mzito kwa wote serikali ya Sudan Kusini na waasi . Marekani imetishia vikwazo vya kusafiri na fedha kwa wale waliohusika na ghasia zilizopelekea zaidi ya watu milioni moja kupoteza makazi.

Akiwa katika mji mkuu wa Ethiopia Kerry atafanya mazungumzo na maafisa wa Umoja wa Afrika juu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo waislam wanaendelea kukimbia makazi yao kuepuka mashambulizi ya wanamgambo wa kikristo.

Pia anatarajiwa kukutana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ili kuzungumzia mapigano dhidi ya wanamgambo wenye mahusiano na Al-qaida Al-shabab.

Jumamosi waziri Kerry ataelekea mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, kukutana na rais Joseph Kabila . Watazungumza juu ya mafanikio ya hivi karibuni ya usalama dhidi ya makundi ya waasi huko mashariki mwa Congo.

Jumapili Kerry ataelekea Angola kwa ajili ya kukutana na rais wa muda mrefu Jose Eduardo dos Santos. Anarudi Washington Jumatatu, Mei 5.
XS
SM
MD
LG