Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 15:53

Balozi Powers atoa wito wa vikwazo Sudan Kusini.


Mlinda amani wa Umoja wa akiwa kwenye doria katika mji wa Malakal, katika jimbo la Upper Nile .
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Samantha Power ameitaka jumuiya ya kimataifa kuwawekea vikwazo wale wanaowalenga raia au wanaoleta mvurugano wa kisiasa Sudan Kusini.

Power alishiriki kwenye mkutano muhimu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa jumatano juu ya hali ya Sudan Kusini. Wanadiplomasia hao walionyeshwa kile Power alichokiita picha za kinyama za mauaji ya wiki iliyopita katika mji wa Bentiu.

Ofisi ya umoja wa mataifa Sudan Kusini inasema waasi wameuwa mamia ya watu kutokana na utaifa au makabila yao baada ya kuchukua udhibiti wa Bentiu Aprili 15. Msemaji wa waasi amekanusha kufanya mauaji hayo.
XS
SM
MD
LG