Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 19:11

Zaidi ya watu 50 wauwawa Nigeria mwishoni mwa juma.


Kituo cha mabasi cha Nyanya kilicholipuliwa mwishoni mwa juma huko Nigeria.
Kituo cha mabasi cha Nyanya kilicholipuliwa mwishoni mwa juma huko Nigeria.
Watu wengi wanahofiwa kupoteza maisha yao baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi nje kidogo ya mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Taarifa za awali zinasema watu wapatao 20 wameuwawa huku wengi wengine wao wakiwa wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali za mji huo kufuatia mlipuko katika kituo cha basi cha Nyanya wakati watu watu hao wakielekea makazini Jumatatu.

Hakukuwa na madai ya mara moja ya kuhusika na mlipuko huo, lakini kundi la wanamgambo wa kiislam la Boko Haram linashukiwa kuhusika na mlipuko huo ambao siku zote hushambulia maeneo ya umma.

Wanamgambo hao wanashukiwa na mashambulizi ya mwishoni mwa juma ambayo yaliuwa watu wasiopungua 60 katika jimbo la Borno. Gazeti moja la Nigeria linaripoti kwamba washambuliaji walishambulia vijiji viwili usiku na kuuwa wakazi majumbani mwao na kuchoma moto majumba na maduka.
XS
SM
MD
LG