Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:56

Imam Makaburi auwawa Mombasa


Shiekh Abubakar Shariff Ahmed, aka, Makaburi auliwa karibu na Shimo la Tewa Mombasa April, 2 2014
Hali ya wasi wasi imetanda huko Mombasa kufuatia kifo cha Sheikh Abubakar Shariff Ahmed, maarufu kwa jina la Makaburi aliyewekewa vikwazo na Marekani na Umoja wa mataifa kwa msimamo wake wa kuunga mkono kundi la Al-Shabab, pamoja na kuwaandikisha vijana kujiunga na kundi hilo. makaburi amekuwa akikanusha tuhuma hizo. .

Polisi inaeleza kwamba mauaji hayo yaliofanywa na watu wasiojulikana wenye silaha yametokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kwamba imeanza operesheni ya kuzuia wimbi la mashumbilizi nchini humo, na kwamba maafisa wa polisi wamewakamata zaidi ya watu 650 huko Nairobi kufuatia milipuko mitatu ya bomu mjini Nairobi siku ya Jumatatu.
please wait

No media source currently available

0:00 0:08:35 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakili wa Imam Ahmed, Mbugua Murithi amesema Sheikh Ahmed aliuwawa pamoja na mtu mwingine asiyejulikana karibu na jela ya Shimo la Tewa nje ya mji wa Mombasa.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Amin Mwidau, mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Toronto Canada, anasema ni kitendo cha kusikitisha lakini anasema mauaji hayo yanatishia kuleta ghasia za kulipiza kisasi.

Mwidau anasema hatari iliyopo kutokana na mauwaji yake kuna uwezekano wa wafuasi wake na watu wengi kuamini zaidi mawaidha yake kwamba waislamu wa Pwani Kenya wanakandamizwa.

Makaburi ni Imam wa tatu kuuliwa Mombasa katika kipindi cha chini ya miezi 6.
XS
SM
MD
LG