Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:33

Uchunguzi wa ndege iliyopotea ya Malaysia umepanuliwa.


Waziri wa muda wa usafirishaji wa Malaysia Hishamuddin Hussein, akizungumza na waandishi wa habari Jumapili, March 16, 2014.
Waziri wa muda wa usafirishaji wa Malaysia Hishamuddin Hussein, akizungumza na waandishi wa habari Jumapili, March 16, 2014.
Serikali ya Malaysia imetoa wito wa kuwepo na uratibu wa kimataifa kutafuta ndege ya shirika la ndege la malysia iliyopotea kwa wiki moja sasa kuanzia bahari ya Caspian hadi kusini mwa bahari ya hindi.

Maafisa wa malysia wanasema idadi ya mataifa ambayo uchunguzi unafanyika imeongezeka kutoka 14 kufikia 25.

Zaidi ya hayo inaripotiwa kwamba Uchunguzi juu ya kupotea kwa ndege ya Malaysia ikiwa na abiria 239 hivi sasa pia unaelekezwa kwa wafanyakazi wa ndege hiyo na abiria.

Maafisa wa Malaysia wanasema Jumapili kwamba polisi wamefanya upekuzi kwenye nyumba za marubani wa ndege hiyo, na pia wanachunguza mtambo wa mazoezi ya kurusha ndege kutoka nyumba ya mmoja wa marubani hao . Maafisa pia wanawafanyia mahojiano wahandisi ambao walikagua ndege hiyo kabla ya kuondoka Kuala Lumpur.
XS
SM
MD
LG