Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 18:32

Kaimu rais wa Ukraine atia saini kufuta kura ya maoni.


Waandamanaji wakibeba mabango wakati wa maandamano ya kupinga vita mbele ya jengo la ubalozi wa Russia huko Kyiv.Machi 7, 2014.
Waandamanaji wakibeba mabango wakati wa maandamano ya kupinga vita mbele ya jengo la ubalozi wa Russia huko Kyiv.Machi 7, 2014.
Kaimu rais wa Ukriane Oleksandr Turchynov ametia saini amri ya kufuta kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Crimea kutaka kujiunga na Russia, lakini maafisa wa Crimea wameapa kuendelea na mpango wao.

Rais Turchynov alitia saini amri hiyo Ijumaa siku moja baada ya bunge la Crimea linaloungwa mkono na Russia kupiga kura kutaka eneo lao kuwa sehemu ya Russia na kuitisha kura ya maoni hapo marchi 16.

Kaimu waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk akisema Ijumaa kwamba hakuna yeyote katika dunia iliyostarabika atakayetambua matokeo ya kura ya maoni ya eneo hilo. Ukraine na Russia zinavutana tangu majeshi ya Russia kuingia katika peninsula Crimea wiki moja iliyopita.
XS
SM
MD
LG