Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 20:13

Majibu ya Republicans kuhusu hotuba ya rais Obama.


Rais Barack Obama akihutubia taifa.
Mjumbe wa baraza la wawakilishi Cathy Morris wa Jimbo la Washington ameelezea kile alichokiita fursa ya kutokuwa na usawa wakati akitoa jibu la Warepublikan kwa hotuba ya hali ya kitaifa ya rais Barack Obama.

Badala yake anasema Bw.Obama amelenga kwenye kutokuwa na usawa katika mapato na kwamba sera za utawala wake zinazidi kuongeza nafasi kati ya maisha ya watu yalipo sasa na wanapotaka yawe.

Mjumbe huyo anasema warepublikan wana mpango wa kuongeza ajira bila kuongeza matumizi ya serikali na kuongeza mipango ya elimu na mafunzo ili kuwatayarisha watu na ajira.

Aliongeza pia kuwa warepublikan wanataka wafanyakazi wapate fedha zaidi katika mishahara yao kupitia punguzo la kodi na gharama nafuu za nishati na afya.

Rais barack obama alihutubia taifa mbele ya bunge Jumanne usiku kuelezea kuhusu taifa linavyoendelea pamoja na mikakati yake ya baadae.
XS
SM
MD
LG