Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:42

AU yaondoa vikwazo dhidi ya Madagascar.

Rais Hery Rajaonarimampianina wa Madagascar akisalimia umati wa watu wakiwa na mke wake wakati wa kampeni za uchaguzi huko Antananarivo, Madagascar, in October 2013.
Rais Hery Rajaonarimampianina wa Madagascar akisalimia umati wa watu wakiwa na mke wake wakati wa kampeni za uchaguzi huko Antananarivo, Madagascar, in October 2013.
Umoja wa Afrika umeondoa vikwazo dhidi ya Madagascar na kusema nchi hiyo imekamilisha kipindi chake cha mpito na kurudisha utawala wa kikatiba.

Baraza la Amani na Usalama la AU liliamua Jumatatu kumaliza marufuku hiyo iliyowekwa baada ya mapinduzi ya mwaka 2009 na kuikaribisha Madagascar kurudi mara moja kwenye ushiriki wake.

Rais Hery Rajaonarimpianina alichukua madaraka Jumamosi baada ya kushinda uchaguzi mwezi Desemba.

Umoja wa Afrika ulitaja uchaguzi wa rais na wabunge katika maamuzi yake ya Jumatatu, wakionyesha shukrani kwa watu wa Madagascar kwa hatua iliyojumuisha watu wote, yenye kuaminika na iliyo ya halali.
XS
SM
MD
LG