Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 07:43

Mbunge Mutambu asema mabadiliko ya katiba yahitajika Kenya


 William Ruto mgombea mwenza wa kundi la Jubilee akihutubia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara Nairobi
William Ruto mgombea mwenza wa kundi la Jubilee akihutubia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara Nairobi
Mabaraza ya baadhi ya wilaya za Kenya zinazojulikana kama County, yamepitisha bajeti wiki iliyopita, zinazongeza bei za bidhaa muhimu na kodi katika juhudi za kukusanya mapato zaidi ya kuendesha shughuli za serikali zao.

Uwamuzi huo umezusha hasira miongoni mwa wananchi na wafanyabishara waloandamana katika miji mbali mbali ya nchi hiyo wiki iliyopita, kulalamika dhidi ya maamuzi hayo na kutaka mabadiliko yafanyike.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wachambuzi na wanasiasa wametoa wito wa kufanyika mageuzi ya katiba ili kupunguza County zilizopo. Wanadai kwamba County hizo zinatumia fedha nyingi kulipa mishahara ya watumishi wa serikali badala ya miradi ya maendeleo, na kuna serikali nyingine zinashindwa hata kuwalipa mishahara watumishi wao.
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mbunge wa Mwingi Central, County ya Kitui Joe Mutambu, akizungumza na Sauti ya Amerika anasema atawasilisha pendekezo la mabadiliko ya katiba bunge likifunguliwa mapema mwezi Februari.

Anasema mabadiliko hayo ni muhimu hivi sasa kutokana na shida zinazotokana na baadhi ya vifungu vya katiba, akisema hawawezi kusubiri hadi madhara yanakuwa makubwa zaidi.

"Shida zimajaa chungu nzima. Tunangojea tukiona, wewe utachomeka na moto, urudishe tena kidole uchomeke tena, ukifikiria au kusema tuko na wakati mchache. Itakuaje, tuko na wataalamu wanaotoa onyo kila siku, sasa tunataka kupewa onyo nyingine gani?"

Bw. Mutambu anasema akikosa uungaji mkono wa wabunge wenzake atakwenda kwa wananchi na kutayarisha kura ya maoni na uwamuzi wao ndio utaamua njia ya kufuata.
XS
SM
MD
LG