Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 22:04

Lupita, Abdi wateuliwa katika tuzo za Oscars.


Lupita Nyong'o katika filam 12 Years a Slave.
Lupita Nyong'o katika filam 12 Years a Slave.
Wacheza sinema wawili kutoka Afrika Mashariki, Lupita Nyong’o wa Kenya na Barkhad Abdi wa Somalia wameteuliwa katika tuzo za sinema – Oscars – zitakazofanyika Machi 2 Hollywood, Marekani. Mwanadada Lupita Nyong’o ameteuliwa kama muigizaji wa pili kwa upande wa wanawake (Supporting Actress) kwa uchezaji wake katika sinema ya “12 Year a Slave” na Abdi, Msomali mwenye makazi yake hapa Marekani, ameteuliwa kama muigizaji wa pili kwa upande wa wanaume (Supporting Actor) katika sinema ya “Captain Phillips.”
Nyong’o alipata sifa kemkem kwa jinsi alivyocheza kama msichana mtumwa katika sinema hiyo ambayo ilikuwa inahusu Mmarekani mweusi aliyekuwa huru lakini akahadaiwa na kuuzwa katika utumwa. Wiki hii Nyong’o alikuwa mmoja wa wanawake waliong’ara katika tuzo za Golden Globe award huko Hollywood ambako sinema ya “12 Years a Slave” alijizolea tuzo mbali mbali.
Nyong’o atakumbukwa kwa uchezaji wake mzuri katika mfululizo wa tamthiliya ya MTV Shuga iliyofanyika Nairobi, Kenya, na kurushwa hewani mwaka 2009 katika nchi kadhaa za Afrika. Katika MTV Shuga Nyong’o na waigizaji wengine vijana wa Kenya waliigiza katika aina mbali mbali kuonyesha hatari za kuambukizana virusi vya HIV katika maisha ya kila siku ya vijana barani Afrika.
XS
SM
MD
LG