Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 11:27

Kesi ya rais wa zamani wa Misri yaahirishwa tena.


Rais wa Misri Mohammed Morsi.
Kesi dhidi ya rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi ilitakiwa kuanza tena Jumatano, lakini ikaahirishwa hadi Februari mosi, kutokana na hali mbaya ya hewa nchini humo, iliyomzuia kupelekwa mahakamani.

Kesi yake inasikilizwa katika chuo cha polisi mjini Cairo, lakini Morsi anashikiliwa katika mji wa Alexandria, yapata kilomita 175, ambako ukungu mzito ulizuia helikopta yake kuondoka Jumatano.

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mwanzo mwezi Novemba mwaka jana ilisikilizwa kwa dakika chache baada ya Bw. Morsi kupinga akisema yeye ndiye rais halali wa Misri.

Misri ilimtimua madarakani mwezi Julai baada ya maandamano ya upinzani, uliomshtumua kwa kudhibiti mamlaka. Zaidi ya watu elfu moja wameuawa, wengi wao wafuasi wa mosri huku maandamano yakiendelea .
XS
SM
MD
LG