Rais wa sudan Omar al-Bashir yuko Juba mji mkuu wa Sudan Kusini kwa ajili ya kujadiliana kuhusu ghasia zinazoendelea katika taifa hilo wakati wapatanishi wa rais Salvar Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wanashindwa kufanya mazungumzo ya amani yenye matokeo mazuri huko Ethiopia.
Waziri wa habari wa Sudan Ahmed Bilal ameiambia Sauti ya Amerika kwamba nchi yake ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ilivyo lakini anadhani kwamba bwana Bashir anaweza kutoa mchango kusaidia pande zote mbili za Sudan Kusini kutafuta suluhu.
Mashauriano ya kumaliza mapigano yaliyozuka katikati ya mwezi Desemba yalitarajiwa kuanza Ethiopia wiki iliyopita lakini wajumbe hawakuweza kufikia makubaliano ya masuala ya madai ya waasi ya kuachiliwa wafungwa wa kisiasa.