Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:31

Mazungumzo ya usuluhishi Sudan Kusini kuanza alhamisi.


Mpinzania wa rais Salva Kiir aliyekuwa makamu rais Rick Machar Riek Machar.
Wajumbe kutoka pande mbili zinazopingana wamekutana nchini Ethiopia kwa mazungumzo ya amani kufuatia wiki kadhaa za ghasia ambazo zimepelekea zaidi ya watu 1,000 kuuuwawa.

Wawakilishi wa Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar waliwasili katika mji mkuu wa Addis Ababa Jumatano.Mwandishi wa VOA Marthe Van Der Wolf ambaye amezungumza na wajumbe amaesema mazungumzo hayo yataanza mapema iwezekanavyo Alhamisi.

Hakukuwa na mapighano mengine jumatano kati ya majeshi ya serikali na yale yanayomuunga mkono Rick Machar huko Bor, mji mkuu wa makao makuu ya jimbo la Jonglei la Sudan Kusini. Katika ujumbe wa Twitter serikali imesema majeshi yake yalijiondoa kwa kiasi fulani huko Bor lakini bado kulikuwa na mapigano mijini.
XS
SM
MD
LG