Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 19:08

Wanamgambo washambulia walinda amani Bangui.


Wakazi wa Damara, kilometa 75 Kaskazini mwa Bangui, wakiondoka eneo hilo December 3, 2013.
Wakazi wa Damara, kilometa 75 Kaskazini mwa Bangui, wakiondoka eneo hilo December 3, 2013.
Umoja wa Afrika umesema wapiganaji ambao wengi wao ni wakristo wanaowapinga wanamgambo wa Balaka walishambulia walinda amani wa Umoja wa mataifa jumatano na kuuwa watu sita.

Wafanyakazi wa huduma wanasema wamegundua dazeni ya miili katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo mapigano yanayohusisha vikundi vyenye silaha yaliongezeka wiki hii.

Chama cha Msalaba mwekundu kimeeleza alhamisi kimegundua zaidi ya miili 40 kutoka mitaa ya Bangui katika siku mbili zilizopita chama hicho kinaeleza kwamba waathirika wengi walikuwa ni raia .
XS
SM
MD
LG