Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 06:48

Uganda yakanusha kumsaidia rais Salva Kiir.


Salva Kiir Mayardit, Rais wa serikali ya Sudan Kusini, Feb 8, 2011 (file photo)
Uganda imekanusha, ripoti kwamba serikali ya nchi hiyo ilipeleka vikosi vya kijeshi vya UPDF kwenda kumsaidia rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika mzozo unaoendelea Sudan Kusini. Msemaji wa wizara ya masuala ya nchi za nje wa Uganda Fred Opolot amesema vikosi vya Uganda Peoples Defense Forces (UPDF) vitapelekwa wiki hii kujaribu kuokoa takriban raia elfu mbili wa Uganda ambao wamekwama katika mapigano nchini humo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Uganda Bw. Opolot amesema wasiwasi wao mku ni kuhakikisha raia wako salama amesema "wasiwasi wetu mkubwa ni kuhakikisha kwamba raia wako salama na iwapo hawana usalama basi tuwaokowe. Utaratibu huo bado unaendelea.

Bw. Opolot amesema vikosi vya UPDF viko mjini Juba kudhibiti uwanja wa ndege ili kuhakikisha utaratibu wa uokozi unakwenda vizuri.

Ghasia nchini Sudan Kusini zilianza baada ya rais Salva Kiir anayetoka kabila la Dinka, kumshutumu makamu wake wa zamani Riek Machar anayetoka kabila la Nuer kwa jaribio la kufanya mapinduzi. Bw. Machar ambaye yuko mafichoni, alikana tuhuma hizo. Na Mzozo huo, unaripotiwa umesasababisha vifo vya zaidi ya watu mia tano na kuwalazimisha maelfu ya wengine kutoroka makazi yao.

Opolot alisuta tuhuma kwamba rais Yoweri Museveni wa Uganda anamsaidia kiongozi wa Sudan Kusini katika mzozo huo amesema "tuhuma hizo hazina msingi. tuna raia wengi wa Uganda huko Sudan kusini na usalama wao ndilo jambo muhimu kabisa kwetu sisi kwa wakati huu, na ndio tunazingatia. Hivyo basi, habari za kuwa wanajeshi wa UPDF kuwa Sudan kusini kumsaidia Rais Kiir hazina ukweli wowote.

Siku ya Ijumaa Rais Barack Obama alipeleka wanajeshi 45 wa Marekani kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi wa kimarekeni na watumishi wa ubalozi wa Marekani. Katika taarifa iliyotolewa na White House mwishoni mwa wiki, rais Obama alisisitiza umuhimu wa shughuli za uokozi za Marekani na kusema viongozi wa Sudan Kusini wanajukumu la kusaidia juhudi hizo.

Bw. Opolot anasema serikali ya Kampala inahakikisha raia wote waliokwama kutokana na mzozo huko Sudan Kusini wako salama na watawaokoa wale walIoathirika moja kwa moja kutokana na mzozo huo. Alielezea wasiwasi juu ya raia wa Uganda walokwama katika jimbo la Jonglei kwenye kambi ya umoja mataifa ambako kumeripotiwa kutokea mapigano makali.

Bw. Opolot anasema Uganda inataka kuwa sehemu ya suluhisho kusaidia kutatua mzozo wa Sudan Kusini. Anasema tangu kuibuka kwa matatizo huko rais Museveni amejaribu kufanya majadiliano na rais Salva Kiir. Anasema waziri wa Uganda wa Uhusiano wa kimataifa ni mmoja kati ya wajumbe wa Umoja wa Afrika waliofanya mikutano kadhaa na pande zote kwenye mzozo huo katika juhudi za kupata suluhisho kwa mzozo huo.
XS
SM
MD
LG