Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 08:37

Marekani , Ulaya zalaani ukandamizaji huko Ukraine.


Mkuu wa sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton akiwa waziri wa zamani wa fedha wa Ukraine.
Marekani imejitokeza na kutoa maoni yake kutokana na malalamiko hayo ya wapinzani wa Ukraine. Hii inafuatia hasa majeshi ya usalama kujaribu Jumanne usiku kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji na jana yamerudi nyuma kutoka kwenye kambi ya waandamanaji katika uwanja mkuu wa kati wa mji mkuu wa Ukraine.

Mvutano kati ya makundi hayo ulianza mapema alfajiri jana ndani ya ukumbi mkuu wa jiji la Kyiv City Hall saa kadhaa baada ya maaskari kuvamia kambi ya waandamanaji katika uwanja wa uhuru wa Kyiv na kubomoa hema zilizowekwa na waandamanaji.

Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych baadae akatoa ahadi kuwa hatotumia nguvu dhidi ya waandamanaji na kuwataka wapinzani kukutana naye kwa mazungumzo.
Upinzani umerudia mara kadhaa kueleza kwamba hautakubali majadiliano yeyote hadi rais aivunje serikali yake awaachie waandamanji walio kizuizini na kuwaadhibu Polisi wa kutuliza ghasia waliohusika na ghasia dhidi ya waandamanaji.

Ombi la Bw. Yanukovych limetolewa baada ya mkutano wake na naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Viktoria Nuland na mkuu wa sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton ambao walikuwa Kyiv kama sehemu ya kusukuma kutafuta kutanzua mzozo huo.

Bi. Nuland aliyezungumza na waandamanaji jana alisema alimlalamikia rais wa Ukraine Yanukovych kuhusu kutumia nguvu za polisi. Na anasema amemueleza bayana kwamba kilichotokea jumanne usiku kwa upande wa usalama haikubaliki katika taifa la ulaya na taifa la kidemokrasia.
XS
SM
MD
LG