Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:15

Kura za uchaguzi wa wabunge bado zinahesabiwa Mali.


Mmoja wa wapiga kura wa kabila la Tamacheq akiwekwa wino baada ya kupiga kura.
Mmoja wa wapiga kura wa kabila la Tamacheq akiwekwa wino baada ya kupiga kura.
Maafisa wa uchaguzi huko Mali wanahesabu kura baada ya uchaguzi wa bunge ambao wapiga kura hawakujitokeza kwa wingi na kuna ripoti za kuwepo na kasoro katika baadhi ya vituo vya kupiga kura.

Uchaguzi wa Jumapili unalengo la kukamilisha hatua ya mwisho ya kujaribu kurudisha tena utawala wa kidemokrasia nchini humo baada ya wanajeshi kumpindua rais mwaka jana na wanamgambo wenye mahusiano na Al-qaeda kuchukua udhibiti wa maeneo ya kaskazini.

Abdel Fatau Musah mkurugenzi wa mahusiano ya nje wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, ameiambia VOA kwamba kulikuwa na kasoro fulani lakini wafuatiliaji hawajaripoti matatizo makubwa .

Hata hivyo amesema uchaguzi uligubikwa na kile alichokiita kitendo cha aibu cha watu wachache kujitokeza kupiga kura.

Maafisa wanasema Watuareg wanaotaka kujitenga waliwazuia wapiga kura katika maeneo machache, huku watu wenye silaha waliiba baadhi ya masanduku ya kura karibu na mji wa kaskazini wa Timbuktu.

Kiasi ya wamali milioni 6.5 wanahaki ya kupiga kura, kukiwa na wagombea zaidi ya 1000 wanaogombania viti 147 vya bunge jipya.
XS
SM
MD
LG