Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 07, 2023 Local time: 16:45

Wengi wahudhuria maziko ya mtangazaji wa kimataifa Annie Idrissu, Dar es Salaam.


Mtangazaji wa kimataifa Ann Idrissu.
Mtangazaji wa kimataifa Ann Idrissu.
Mfanyakazi wa zamani wa Idhaa ya Kiswahili ya VOA Bi. Annie Nendiwe Iddrisu amezikwa Jumatatu huko Kinondoni Dar es Salaam, Tanzania katika mazishi yaliohudhuriwa na watu wengi hasa waandishi wa habari.

Bi. Idrissu alifariki dunia Jumanne iliyopita katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mama Anna Iddrissu aliwahi kufanya kazi Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) katika miaka ya 70 hadi 90.

Kabla ya kuwasili Washington alikuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Ghana huko Accra na baada ya kustaafu VOA Bi Idrissu alirudi nyumbani Tanzania na kuanzisha studio yake ya kutayarisha vipindi vya maswala vya kijamii “Power House Production”, ambapo alitengeneza vipindi vya afya na jamii akishirikiana na Channel 10 na pia kipindi maarufu cha "Tikisa" kilichokuwa kikirushwa na kituo cha ITV. Marehemu Idrissu ameacha watoto wawili na wajukuu wanne. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amen.
XS
SM
MD
LG