Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 23:51

Washukiwa wanne wafikishwa mahakamani Kenya.


Mtu mwenye silaha wakati wa mashambulizi ndani ya maduka ya kifahari ya Westgate mall Kenya. Reuters on Oct. 17, 2013.
Maafisa huko Kenya wamewashitaki watu wanne kuhusiana na mashambulizi kwenye maduka ya kifahari ya Nairibi ya Westgate ambayo yalisababisha vifo vya watu 67.

Washukiwa haoMohamed Ahmed Abdi, Liban Ibrahim na Hussein Hassan wote walikana makosa katika mahakama moja ya Nairobi.

Hakuna kati ya hao wanao shikiliwa, wanashutumiwa kuwa ndio washambuliaji ya mwezi Septemba huko West gate . Hata hivyo wanashitakiwa kwa kufanya kitendo cha kigaidi kwa kuwapa makazi watu wanaoshutumiwa kuwa ni washambuliaji.

Mashitaka mengine ni pamoja na vitambulisho vya uongo na kuishi Kenya kinyume cha sheria.
XS
SM
MD
LG