Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:28

Majeshi ya serikali ya Congo yakomboa mji wa Bunagana.


Makamanda wa jeshi la Congo wakipanga mikakati.
Makamanda wa jeshi la Congo wakipanga mikakati.
Jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya Congo limefanikiwa kuuteka mji wa mpakani na Uganda wa Bunagana ngome ya mwisho iliyobaki ya kundi la waasi wa M23. Maafisa wa serikali na mashahidi wanasema majeshi ya serikali yaliingia katika mji huo baada ya wapiganaji wa M23 kuondoka huko.

Kundi hilo la waasi liliuteka mji wa Bunagana na miji mingine ya jimbo la Kivu Kaskazini la Mashariki ya Congo lilipoanza uasi wake mwaka jana. Kumekuwa na mapigano makali kuanzia siku ya Ijumaa wakati majeshi ya serikali ya Congo yakisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa kuanzisha mashambuklizi ya kukomboa miji hiyo inayoshikiliwa na waasi.

Idara ya Umoja wa Mataifa inayowahudumia wakimbizi – UNHCR, inaeleza kwamba mapigano yamesababisha maelfu ya wakongo kukimbilia Uganda.
XS
SM
MD
LG