Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 07:04

Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba Tanzani kurudishwa bungeni.


Mgombea wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza rais Jakaya KIkwete alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 31 2010.
Mgombea wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza rais Jakaya KIkwete alipotangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 31 2010.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana kuwa kuna upungufu katika sharia ya mabadiliko ya katiba walipokutana Jumanne katika Ikulu ya Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao uliitishwa na Rais Kikwete ulitokana na wabunge wa vyama upinzani kutoa kauli ya kutaka kuandamana baada ya bunge kupitisha mswaada wa sheria ya mabadiliko ya katiba bunge lilipokutana Dodoma mwezi Septemba.
Rais Kikwete alikubali kwamba lazima wakae wazungumze akitolea mfano wa siku za nyuma.
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na sauti ya Amerika mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema Freeman Mbowe amesema Rais Kikwete ametoa mwito wa kutafuta ufumbuzi wa pamoja na ndicho walichofanya huko Ikulu.

Mambo ya msingi waliyokubaliana ni kwamba sheria ina mapungufu na itabidi wairudishe bungeni ifanyiwe mabadiliko.

Wamekubaliana pia wasikilize maoni ya wadau wa Zanzibar. Kuhusu hoja ya mchakato wa katiba uwe shirikishi na usihodhiwe na chama chochote cha siasa, sababu tabia ya wabunge wa CCM kujiona wana haki ya ziada kuliko raia wengine kuhodhi mchakato wa katiba haukubaliki kwani inaweza kupelekea taifa kwenye machafuko.
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wabunge wa vyama vya Chadema ,CUF na NCCR Mageuzi walisusia mjadala wa mswaada huo wakipinga kuwa utaratibu uliotumika haukushirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya mswaada huo.
XS
SM
MD
LG