Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:02

Jaji Warioba awapa onyo wanasiasa wa Tanzania.


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania
Tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania imeonya wanasiasa nchini humo kutovuruga mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na kusema kwamba maridhiano ya pamoja ya kitaifa ndiyo yatakayoleta katiba itakayokubalika na watanzania wote

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Alhamisi kuelezea hatua ya sasa ya mchakato wa upatiakanaji wa katiba mpya Tanzania ambapo sasa tume inakaa kama kamati kuchambua maoni yaliyotokana na mabaraza ya katiba ili kutengeneza rasimu ya pili ya katiba itakayowasilishwa kwenye bunge maalum.

Kauli ya jaji warioba imekuja huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka vyama vitatu vya upinzani vya NCCR MAGEUZI, CHADEMA na CUF ambapo kwa sasa viongozi wake wakuu wanazunguka kufanya mikutano ya hadhara maeneo mbalimbali nchini kupinga sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2013 na kumtaka Rais Jakaya Kikwete asitie saini kutokana na mapungufu waliyoainisha kubwa likiwa ni mchakato wa upatikanaji wa bunge maalum la katiba na Zanzibar kutoshirikishwa.

Jaji Warioba ameshauri watanzania kukaa pamoja kutafakari tofauti zao ili kufikia muafaka wa katiba ipi wanaitaka na kwamba katiba mpya haiwezi kupatikana kwa malumbano ya wanasiasa au maandamano na mikutano ya hadhara

Amelaumu utaratibu wa baadhi ya wanasiasa katika majukwaa kuzungumza masuala yenye maslahi yao na kuwagawa watanzania ambapo amesema hata kweye rasimu ya kwanza ya katiba masuala ya utaifa yote yamezungumzwa na wananchi katika maoni yao waliyoyatoa sehemu mbalimbali nchini

Hata hivyo jaji Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania Jaji warioba ametaka bunge litafakari upya kipengele cha kuvunjwa tume yake mara baada ya kukabidhi rasimu ya pili ya katiba kwenye bunge maalum, Kwavile tume ya mabadiliko ya katiba inatakiwa kurudi tena kwa wananchi kuwaelimisha kuhusu upigaji wa kura ya maoni ambayo ni hatua ya mwisho ya upatikanaji wa katiba mpya. sula hili pia linaendana pia na madai ya wanasiasa wa upinzani wanaopinga kuvunjwa kwa tume hiyo.

Kwa mujibu wa sheria, mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya Tanzania unatakiwa kukamilika ifikapo April 26, 2014,
XS
SM
MD
LG