Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 13:00

Ban kuwasilisha ripoti ya wachunguzi wa silaha za kemikali Syria.


UN-Syria-Chemical-Weapons
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon ataliarifu baraza la usalama hii Jumatatu juu ya kile wakaguzi wa silaha za kemikali walichogundua baada ya kufanya uchunguzi huko Syria.

Timu hiyo ilichukua sampuli ya mchanga kutoka kwenye mitaa ya Damascus na sampuli za damu kutoka kwa raia waathirika wa mashambulizi ya gesi ya sumu mwezi uliopita.

Kazi yao ilikuwa si kuangalia nani wa kulaumiwa lakini kuthibitisha shambulizi kutokea. Lakini Marekani inasema hakuna shaka yeyote kwamba jeshi la Bw. Bashar Al Assad limehusika.
XS
SM
MD
LG