Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 02:26

Ibrahim Keita aapishwa kuwa rais mpya wa Mali.


Ibrahim Boubacar Keita akizungumza na waandishi huko Bamako.
Ibrahim Boubacar Keita ameapishwa kuwa rais mpya wa Mali baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza nchini humo tangu mapinduzi ya mwaka jana.

Bw.Keita aliahidi kulinda mafanikio ya kidemokrasia na kuahidi kujenga umoja wa kitaifa wakati wa hafla ndogo leo jumatano katika mji mkuu Bamako.

Rais huyo mpya pia aliahidi kupambana na rushwa akisema hakuna atakayepata utajiri kutokana na fedha za umma tena.

Sherehe kubwa itakayohudhuriwa na viongozi wa dunia inatarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.

Bw.Keita ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu na rais wa bunge la taifa alishinda uchaguzi wa Agosti 11 kwa kupata asilimia 77 ya kura. Ushindi wake pia ulitokana na kuungwa mkono na viongozi wa dini ya kiislam, jeshi na wengi wa wapinzani wake wa uchaguzi wa duru ya kwanza.
XS
SM
MD
LG