Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 06:52

Rwanda yaongeza ushuru wa mpakani na Tanzania kwa zaidi ya asilimia 200.


Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rwanda imeamua kupandisha ushuru wa magari ya mizigo kutoka dola za Marekani 152 hadi 500 kuanzia tarehe 9 Septemba mwaka huu.

Akizungumza na Sauti ya Amerika waziri wa miundo mbinu wa Rwanda Bw. Silas Gwakabamba alisema ushuru huo mpya ambao ulisababisha mtafaruku katika eneo la Rusumo umesitishwa kwa muda kwa muda ili kuruhusu wafanyabiashara waliokuwa wamekwama mpakani humo kuweza kuendelea na safari zao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Iliripotiwa kuwa magari yapatayo 200 ya mizigo yalikwama katika eneo la Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania baada ya kutangaziwa kodi hiyo mpya , akifafanua hali hiyo waziri huyo wa miundo mbinu wa Rwanda amesema magari hayo yameachiwa kwa sasa.

Waziri ameongeza kumekuwa na mazungumzo kati ya mawaziri wa fedha wa nchi hizo na bei hiyo iliamuliwa na Rwanda kwasababu wao pia walikuwa wakilipishwa dola hizo 500 wakielekea Tanzania, lakini aliongeza anavyoelewa mawaziri walijaribu kukubaliana juu ya msingi wa mahesabu na waziri wao wa fedha ndiye anashughulikia suala hilo.

Na anaamini kuna makubaliano yanayoendelea kati ya serikali hizo ambapo kwa upande wa Mombasa na Kampala tayari wamekubali kuondoa vikwazo vingi barabarani ila upande wa Tanzania bado akiongeza kuwa waziri wa Tanzania tayari ameshafika Rwanda mara mbili kuongelea suala hilo.
XS
SM
MD
LG