Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 13:19

Mwakyembe aahidi kuendelea na vita dhidi ya usafirishaji madawa Tanzania.


Tanzanian minister of Transportation.
Waziri wa uchukuzi wa Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe amehaidi kufichua mtandao wa waliohusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Johanesburg,afrika kusini julai 5 mwaka huu.

Waziri Mwakyembe alisema hayo hii Jumatano alipofanya ziara ya ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ili kujionea namna mamlaka mbalimbali za uwanja zinavyofanya kazi za kupitisha abiria na mizigo.

Dkt.Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madwa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya .

Julai 5 mwaka huu watanzania wawili Agness Gerald na mwenzake Melisa Edward walikamatwa na kuhusishwa na kusafirisha dawa za kulevya za uzito wa kilo 150 zilizokuwa katika mabegi 6 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Or Thambo Afrika Kusini mabegi ambayo yalipita siku hiyo majira ya alfajiri katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere bila ya kukamatwa.

Dkt. Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madawa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya.
XS
SM
MD
LG