Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 03:16

AU: Uchaguzi wa Zimbabwe ulikuwa huru.


Mjumbe wa AU rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo.
Umoja wa Afrika umesema uchaguzi wa Zimbabwe ulikuwa huru na wa haki lakini unataka taarifa zaidi kuhusu matatizo yalioripotiwa.

Olusegun Obasanjo ambaye aliongoza timu ya wafuatiliaji wa Umoja wa Afrika , amesema Ijumaa kwamba kulikuwa na hitilafu ambazo zingeweza kuepukwa .

Obasanjo amesema timu yake imeona idadi kubwa ya wapiga kura ambao walizuiwa kupiga kura. Lakini akaongeza kuwa haamini hali hiyo ilitokea kwingine kuweza kuathiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.

Chama cha rais wa muda mrefu Robert Mugabe kimedai ushindi katika uchaguzi wa Jumatano ingawa matokeo ya mwisho bado hayajatangazwa .

Mpinzani wake waziri mkuu Morgan Tsvangirai jana Alhamis alisema kulikuwa na wizi wa kura na kwmaba uchaguzi huo huashirii matakwa halisi ya wananchi wa Zimbabwe.
XS
SM
MD
LG