Wakati Mali ikihesabu kura baada ya uchaguzi wake wa rais wa Jumapili Waziri mkuu wa Ufaransa Jean Marc Ayrault amesifu uchaguzi huo kuwa wa mafanikio makubwa ambao utaipa Mali kila nafasi ya kuwa taifa huru la kidemokrasia na kuhakikisha maendeleo yake.
Ufaransa iliongoza uvamizi huko Mali baada ya miezi 18 ambayo ilipelekea mapinduzi ya kijeshi na wanamgambo wa kiislam kuchukua upande wa kaskazini mwa nchi.
Mwandishi wa VOA Anne Look anasema maafisa wa uchaguzi wanaripoti kuwa watui wengi walijitokeza kupiga kura na kwamba wananchi wana furaha na matumaini.
Ulinzi ulikuwa mkali na upigaji kura ulikuwa hauna ghasia licha ya vitisho vya Watuareg wanaopigania kujitenga.
Wagombea ni pamoja na mawaziri wakuu wawili wa zamani Ibrahm Boubacar Keita na Modibo Sidibe . Wagombea wengine wa juu ni Soumaila Cisse ambaye aliongoza umoja wa fedha wa Afrika magharibi na mgombea asiyejulikana sana Dramane Dembele ambaye anaungwa mkono na chama kikubwa kuliko vyote huko Mali cha Adema.