Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 03:17

Wagombea urais Mali wafanya mikutano ya mwisho.


Mtuareg akicheza wakati wa kampeni ya urais Mali.
Mtuareg akicheza wakati wa kampeni ya urais Mali.
Wagombea uchaguzi huko Mali wanafanya mikutano yao ya mwisho wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi muhimu wa rais Jumapili.

Wagombea wapatao wanne wanafanya mikutano leo kusini mwa nchi ambako wapiga kura wengi ndiko waliko na ambapo maelfu ya raia wa Mali walikimbilia mwaka jana baada ya wanamgambo kuchukua udhibiti wa kaskazini.

Maafisa wa Mali wamekimbilia kugawa kiasi cha vitambulisho vya kupigia kura milioni 7 kabla ya upigaji kura kuanza. Makosa katika orodha ya wapiga kura na mambo mengine yamechochea shutuma za wizi na kutokuwa na uthabiti.
XS
SM
MD
LG