Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:07

Huduma za simu zarejeshwa katika majimbo yaliokuwa na ghasia Nigeria.


Haya ni baadhi ya majengo yalioungua kutokana na mashambulizi ya Boko Haram huko Kano.
Nigeria imerejesha huduma ya simu za mikononi katika majimbo matatu ambako huduma hiyo ilifungwa ili kuwazuia wanamgambo wa kiislamu kuratibu mashambulizi yao.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Nigeria, chris olukolade ameiambia sauti ya amerika kwamba huduma ya simu za mikononi imejereshwa katika jimbo la borno ijumaa baada ya kuhuduma hiyo kurejeshwa huko yobe na adamawa.

Amesema maafisa wanaamini kuwa hali katika majimbo matatu ya kaskazini mashariki ni thabiti vya kutosha, na watu wanaweza kurejea katika maisha ya kawaida.
Mwandishi wa habari katika jimbo la borno, abdulkareem haruna ameiambia voa kwamba mtandao wa simu za mikononi umerejea kwa kiasi cha saa mbili na halafu umefungwa tena.

Rais goodluck jonathan amepeleka wanajeshi wa ziada kwenye majimbo matatu katikati ya mwezi May baada ya kuongezeka kwa mashambulizi na harakati za kundi lenye msimamo mkali la boko haram, ambalo linalaumiwa kwa maelfu ya vifo katika muda wa miaka minne iliyopita.

Huduma za simu za mkono zilifungwa kuzuia mawasiliano kati ya wapiganaji wa boko haram.
XS
SM
MD
LG