Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:38

Afya ya Mandela yaanza kuwa nzuri akisherekea miaka 95 .


Rais wa zamani na rais mweusi wa kwanza Afrika Kusini Nelson Mandela. (AP Photo/Peter Dejong, file)
Rais wa zamani na rais mweusi wa kwanza Afrika Kusini Nelson Mandela. (AP Photo/Peter Dejong, file)
Afrika kusini imesema afya ya rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela imeanza kuwa nzuri wakati leo anafikisha miaka 95 . Rais Jacob Zuma alituma salamu za pongezi za siku ya kuzaliwa kwa Mandela katika taarifa akisema kuwa Afrika Kusini inajivuna kumwona kiongozi huyo mashuhuri wa kimataifa ni wa kwao. Mtoto wa kike wa Mandela Zindzi Mandela alithibitisha Alhamisi kwamba afya ya baba yake inaendelea kuwa nzuri. Anasema kuna wakati hali yake ilikuwa mbaya na ya kutisha , lakini wiki tatu zilizopita ameonyesha mabadiliko makubwa . Anasema ana uhakika baba yake atarejea nyumba hivi karibuni. Kiongozi huyo mtetezi dhidi ya ubaguzi wa rangi amekuwa katika hospitali mjini Pretoria kwa zaidi ya mwezi mmoja akisumbuliwa na maambukizo kwenye mapafu.
XS
SM
MD
LG