Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:43

Waziri mkuu mpya wa muda aanza kazi Misri.


Rais wa muda Adly Mansour, kulia akizungumza na Hazem el-Beblawi, kushoto huko Cairo, Misri Julai 9, 2013.
Rais wa muda Adly Mansour, kulia akizungumza na Hazem el-Beblawi, kushoto huko Cairo, Misri Julai 9, 2013.
Waziri mkuu wa muda Misri Hazem El Bibawi anaanza kazi Jumatano akiunda baraza lake ambalo televisheni ya taifa ya nchi hiyo inasema ni pamoja na mipango ya kuwapa nafasi wachama wa Muslim Brootherhood na chama cha kiislam cha Nour.

Viongozi wa muda wanaendelea na kipindi cha mpito wa kisiasa Misri ambao unajumuisha hatua za kurekebisha katiba ya nchi hiyo na kufanya uchaguzi mpya wa bunge na rais.

Vyama vya Muslim Brotherhood na Nour ni sehemu ya makundi mengi yanayokosoa mpango huo wa mpito, ambao rais wa muda Adly Mansour aliutoa siku kadhaa baada ya jeshi kumwondoa rais Mohamed Morsi.

Kundi kuu lenye mrengo wa kati National Salvation Front limesema Jumatano kwamba halikushirikishwa na mpango huo na kutokukubaliana na baadhi ya mambo. Kikundi cha vijana cha Tamarud pia kimesema hakikushirikishwa na makundi yote yanapanga kupendekeza mabadiliko kwenye mpango huo.

Chama cha Muslim Brotherhood kinapinga kuundwa kwa serikali ya muda na kutaka Bw.Morsi arudishwe madarakani.Msemaji wa kundi hilo amesma Jumatano kwamba wanakataa mpango wowote wa kujiunga na serikali mpya.
XS
SM
MD
LG