Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:55

AU yaifutia Misri uanachama kwa muda.


Raia wa Misri wakisherehekea baada ya Rais mpya kuapishwa .
Raia wa Misri wakisherehekea baada ya Rais mpya kuapishwa .
Umoja wa Afrika umesimamisha kwa muda uanacchama wa Misri katika umoja wake leo Ijumaa baada ya kutimuliwa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi, kulingana na sheria zake kali dhidi ya mabadiliko ya serikali kinyume cha katiba.

Afisa wa AU amesema Baraza la amani na usalama la umoja huo liliamua kusimamisha ushiriki wa Misri katika shughuli za umoja huo mpaka pale utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa.

Baraza la umoja wa Afrika lilikutana leo katika makao makuu ya AU nchini Ethiopia kujadili mzozo wa kisiasa wa Misri kufuatia kuondolewa kwa Morsi na jeshi siku ya jumatano.

Kutimuliwa kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia hakuendani na vipengele vya katiba ya Misri na badala yake inaangukia katika mabadiliko ya serikali kinyume cha katiba.

Kabla ya mkutano huo kamishna wa AU Nkosazana Dlamini Zuma alisisitiza msingi wa msimamo wa taasisi hiyo kwa mabadiliko kama hayo kwa serikali.

Hata hivyo balozi wa Misri katika umoja wa afrika Mohamed Edress alisema kabla ya maamuzi hayo kwamba sauti za mamilioni ya raia wa Misri lazima zisikike , zieleweke na kuheshimiwa.
XS
SM
MD
LG