Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 23:14

Kenya yakumbwa na mashambulizi ya bomu.


watu wakikimbia baada ya tishio la bomu kutokea katika mtaa wa Earthquake.
Kenya imekumbwa na mfululizo wa mashambulio kadhaa katika mikoa mitatu tofauti.

Mashambulio hayo yameripotiwa kutokea kati ya jumapili usiku na mapema jumatatu ambapo watu wawili wamethibitishwa kufariki na wengine kadhaa wakajeruhiwa.

Katika mji wa Mombasa huko Pwani ya Kenya takriban watu 10 walijeruhiwa jana usiku katika mtaa wa Likoni, kufuatia Gruneti iliyorushwa katika uwanja wa kanisa.

Umati wa watu walikuwa wamekusanyika kwa maombi ya jioni katika kanisa la Earthquake Miracle Ministries, pale mlipuaji aliyekua abiria kwenye pikipiki alipowatupia kifaa kilicholipuka.

Katika mkoa wa Kaskazini Mashariki mlipuko mwingine umewaua watoto wawili, eneo lililo karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Huko Nairobi karibu na mtaa wa Eastleigh watu watano walijeruhiwa katika mlipuko mwingine, uliotajwa kama shambulio la kigaidi.

Afisa mkuu wa jeshi la polisi katika mkoa wa Pwani Aggrey Adoli anasema mtuhumiwa anasakwa na polisi na hali ya usalama katika eneo hilo ni shwari.Amewataka wanachi kutochukulia shambulizi hilo kama ni la kigaidi.
XS
SM
MD
LG